Chama: Yanga Watawafunga Zesco, Wakomae Tu

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Clatous Chama amefunguka kuwa wapinzani wao Yanga wana uwezo mkubwa wa kuwafunga Zesco United kwao lakini wanatakiwa wafanye kazi kubwa kutokana na historia ya Zesco wakiwa kwao.

 

Chama ambaye amewahi kuichezea Zesco United ameweka wazi kwamba Yanga wana nafasi ya kushinda katika mchezo huo lakini wanatakiwa kujitoa kwelikweli kwani Zesco hawana rekodi ya kupoteza wakiwa kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa, Zambia.

 

Yanga itasafiri kuelekea Zambia kwa ajili ya kurudiana na Zesco katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Ukiniambia Zesco na Yanga nani nataka washinde basi ni Yanga. Ndiyo ninataka washinde licha ya kwamba wao ni wapinzani wetu, ninataka washinde ili soka la Tanzania likue zaidi.

 

“Lakini pia kama wanataka kushinda siyo kirahisi kwani wanatakiwa kufanya kazi kubwa kutokana na historia ya Zesco nyumbani,” alisema Chama

Said Ally, Dar es Salaam


Loading...

Toa comment