CHAMBUSO: MUZIKI SIYO WA MKUBWA FELLA!

Meneja wa mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa, Aslay Isihaka ‘Dingi Mtoto’, Chambuso amesema Mkubwa Fella haumiliki muziki wa kizazi kipya kwani kwani hata yeye alizaliwa akaukuta.

“Wanaosema kwamba muziki upo kwa Mkubwa Fella peke yake, kwamba ukianzia kwake na ukatoka basi hautaweza kufanya vizuri tena, wanakosea na hakuna kitu kama hicho.

“Mbona Aslay anafanya vizuri sana na hayupo kwa Fella? Msisahau kwamba hata yeye huu muziki alizaliwa na akaukuta, kivipi ishindikane msanii kutoboa kisa hafanyi kazi naye, hicho kitu sikiamini.”

Chambuso ambaye yeye na Mkubwa Fella ni waanzilishi wa Record Label ya Mkubwa na Wanawe, alikuwa akilisimamia Kundi la Yamoto Band ambalo kwa sasa limebaki stori.

Aliamua kujiengua kwenye lebo hiyo na kuanzisha yake ambayo ina wasanii wachache akiwemo Aslay na Osama.

NA ISRI MOHAMED/GPL

KIMENUKA!! Kumbe Diamond Alizaa Mapacha na Shoga Ake Zari

Loading...

Toa comment