CHAMPIONI LINAVYOMWAGA FEDHA KWA WASOMAJI WAKE!

Moses Mweige wa Mikocheni jijini Dar akionyesha gazeti la Championi lenye Stika ndani yake aliyvyojishindia TSh 10,000.

GAZETI la Championi limeanza kurejesha kidogo linachokipata kwa wasomaji wake, hivyo zawadi kemkemu zitamwagwa.

Msomaji atakayenunua gazeti hili na mengine ya Championi atakuwa na nafasi ya kujishindia fedha taslimu kuanzia shilingi 5,000, 10,000, 20,000, simu za mkononi na zawadi nyingine nyingi.

 

Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatano, Phillip Nkini (kulia) akimkabidhi Moses Mweige wa Mikocheni jijini Dar Sh 10,000 aliyojishindia baada ya kukunua gazeti hilo.

 

 

Unachotakiwa kufanya ni kununua gazeti, fungua ndani kwenye ukurasa mmoja utakuta stika ambayo imebandikwa, ifungue utakuta zawadi yako ndani, baada ya hapo piga simu kwenye namba iliyopo kwenye stika hiyo na ujitambulishe jina, umri, sehemu ulipo na zawadi uliyoshinda.

 

Balari Likong’o wa Mbagala akionyesha gazeti baada ya kujishindia Sh 5,000.

 

Baada ya hapo utapewa maelekezo ya jinsi ya kupata zawadi yako. Angalizo usipoteze gazeti wala kuponi uliyoshinda zawadi hiyo, kadiri unavyonunua magazeti mengi ndivyo unavyopata nafasi ya kushinda zawadi nyingi zaidi.

Nkini akimkabidhi Balari Likong’o wa Mbagala jijini Dar Tsh 5,000 aliyojishindia baada ya kukunua gazeti hilo. PICHA: SWEETBERT LUKONGE.

 

 

 

Hadi sasa washindi watatu wameshajinyakulia zawadi zao za fedha taslimu, ambao ni Nassor Gallu wa Dar aliyejishindia Sh 5,000, Moses Mwaige wa Mikocheni (Sh 10,000), Balari Likong’o wa Mbagala (Sh 5,000), John Bujiku wa Meatu (Sh 10,000) na Malumbano Peter wa Arusha (Sh 10,000).

MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Toa comment