Championi Linazidi Kumwaga Simu na Mkwanja

Mwandishi wa Championi, Sweetbert Lukonge (kushoto) akimkabidhi Erick Msenji wa Tabata Kimanga, Dar Sh 10,000 aliyojishindia baada ya kununua gazeti la Championi.

GAZETI la Championi limeanza kurejesha kidogo linachokipata kwa wasomaji wake, hivyo zawadi kemkemu zitamwagwa.

Msomaji atakayenunua gazeti hili na mengine ya Championi atakuwa na nafasi ya kujishindia fedha taslimu kuanzia shilingi 5,000, 10,000, 20,000, simu za mkononi na zawadi nyingine nyingi.

 

Msomaji atakayebahatika kukuta stika kwenye moja ya kurasa katika gazeti lake alilonunua, atapata zawadi kulingana na maelekezo ya stika hiyo. Stika inaweza kuwa na zawadi ya Sh 5,000 au 10,000 au 20,000 au simu au zawadi nyingine.

Kama gazeti lako ulilonunua halina stika, basi utambue kuwa haujabahatika kupata zawadi, hivyo unatakiwa kuendelea kununua magazeti mengine ya Championi ili kujaribu bahati nyingine.

 

Ukikuta stika kwenye gazeti lako, ifungue utakuta zawadi yako ndani, baada ya hapo piga simu kwenye namba iliyopo kwenye stika hiyo na ujitambulishe jina, umri, sehemu ulipo na zawadi uliyoshinda.

Baada ya hapo utapewa maelekezo ya jinsi ya kupata zawadi yako. Angalizo usipoteze gazeti wala stika uliyoshinda zawadi hiyo, kadiri unavyonunua magazeti mengi ndivyo unavyopata nafasi ya kushinda zawadi nyingi zaidi.

 

Hadi sasa washindi nane wameshajinyakulia zawadi zao za fedha taslimu, baadhi yao ni Nassor Gallu wa Dar aliyejishindia Sh 5,000, Moses Mwaige wa Mikocheni (Sh 10,000), Balari Likong’o wa Mbagala (Sh 5,000), John Bujiku wa Meatu (Sh 10,000), Malumbano Peter wa Arusha (Sh 10,000) Na Erick Msenji wa Tabata, Dar.

MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

Toa comment