The House of Favourite Newspapers

CHAMPIONI, UWAZI YAMWAGA ZAWADI KWA WAUZAJI WAKE

Ofisa Masoko wa Global Publishers,Songoro Bilali (kushoto) akimkabidhi muuzaji wa magazeti, Adam Ally, meza ya kuuzia gazeti eneo la Kagera-Magomeni jijini Dar.

MAGAZETI ya Championi na Uwazi yanayochapishwa na Kampuni kongwe na bora ya Magazeti Afrika Mashariki, Global Publishers jana Jumanne, Januari 29, 2019, yamegawa zawadi za tisheti kwa wauzaji wake na wasomaji wa magazeti hayo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

songoro Bilali (wa tatu kushoto) akimkabidhi fulana ya Gazeti la Uwazi muuzaji wa magazeti, Adam Ally (kulia).

 

Zawadi hizo ni mwendelezo wa promosheni zakeĀ  kabambe ambazo wateja wa magazeti hayo wanajishindia pesa taslim kuanzia Tsh. 10,000 hadi Tsh. 100,000 na wengine wakiibuka washindi wa simu za kisasa kila wiki kwa kununua magazeti hayo, jana yalikuwa kwenye mitaa ya Bunju B, Kigamboni, Mbagala, Gongo la Mboto na Mabibo jijini Dar es salaam ambapo wauzaji wake walipata fursa ya kuzawadiwa tisheti za Championi na za Uwazi.

Ofisa Masoko wa Global, Songoro Bilali (kushoto) akimkabidhi muuza magazeti, Adam Shaban (kulia) wa eneo la Mabibo Dar meza na naironi ya kufunikia magazeti hasa msimu huuu wa mvua.

 

Mbali na tisheti hizo, timu ya masoko ya Global Publishers iliwahamaisha wasomaji wake kununua Championi na Uwazi ambayo ndani yake yanatoa fursa ya msomaji kushinda zawadi hizo.

Ofisa Masoko wa Global, Mussa Mgema (kushoto) akipozi na muuzaji wa magazeti mara baada ya kumkabidhi meza ya kuuzia magazeti eneo la Bunju jijini Dar.

Kwa Championi kuna stika maalum yenye zawadi ambazo ni simu na pesa taslim, hivyo msomaji akinunua gazeti hilo anapaswa kuangalia ndani iwapo atakuta stika ya zawadi ailete ofisini kwetu Sinza Mori akiwa na gazeti lake, ataopewa zawadi ya mkwanja au simu jannja (smartphone) mpya papo hapo.

Muuzaji wa magazeti eneo la Bunju Dar akipozi na gazeti la Uwazi linalozalishwa na Kampuni ya Global Publishers.

 

Kwa upande wa Uwazi, unaponunua gazeti hili kuna kuponi na maelezo ya namna ya kushiriki katika ukurasa wa pili wa gazeti hilo, hivyo unahimizwa kununua Uwazi na kushiriki promosheni hiyo ambayo itakufanya uibuke na mkwanja mrefu hasa katika kipindi hiki kigumu cha mwanzo wa mwaka ambapo hali ya uchumi ni ngumu ama simu janja mpya kwa ajili ya mawasiliano.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Charles Mponzi (kushoto) akimkabidhi muuzaji wa magazeti eneo la Wazo Tegeta Dar Fulana yenye nembo ya gazeti la Championi.

 

Hata wewe unaweza kuwa mshindi, wengi wamekuwa washindi kwa kuchukua uamuzi wa kusoma magazeti yanayochapishwa na Global Publishers.

 

 

Wewe unaweza kujishindia zawadi kemukemu kwa kununua gazeti la Championi na Uwazi, lakini magazeti mengine ya Global Publishers ambayo ni Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda yanakupa nafasi ya kujishindia zawadi za T-shirt, fedha taslimu na zawadi nyingine nyingi ambazo zinapatikana kwa kununua magazeti hayo kwa shilingi mia nane (800) tu, ukajinyakulia zawadi zawadi mbalimbali.

 

Na Musa Mgema, Dar es Salaam

Comments are closed.