The House of Favourite Newspapers

CHAMPIONS LEAGUE: Man U na PSG , Juve na Atletico, Barca, Madrid…!

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya England Manchester City wamepangiwa kucheza na klabu ya Schalke ya Ujerumani katika hatua ya 16 bora Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya droo kufanywa.

Mabingwa hao watetezi wa ubingwa Ufaransa hawajashindwa msimu huu ligini nyumbani ambapo wanaongoza wakiwa na alama 44 kutoka mechi 16. Wana washambuliaji nyota kama vile Neymar, Kylian Mbappe na Edison Cavani.

Walimaliza viongozi Kundi C, kundi ambalo lilikuwa na Liverpool, Napoli na Red Star Belgrade katika hatua ya makundi. Lakini walishindwa na Liverpool uwanjani Anfield.United hawajawahi kukutana na Paris St-Germain katika michuano ya Ulaya.

Hata hivyo, mashetani hao wekundu hawajawahi kushinda na klabu yoyote kutoka Ufaransa katika michuano ya Ulaya tangu mwaka 2005.

 

 

Kwa mashabiki wengi wa Manchester City, wanaonekana kufurahia kukabidhiwa Schalke, ambao kwa kuangalia viwango vya soka ilikuwa ndiyo klabu ‘hafifu’ zaidi ambayo wangekabidhiwa. Schalke wamo nafasi ya 13 Bundesliga na wameshinda mechi nne pekee kati ya 15.

 

Schalke walimaliza wa pili Kundi D nyuma ya Porto lakini mbele ya Galatasaray na Lovomotiv Moscow. Mechi za kwanza zitachezwa 12-13 na 19-20 Februari, na mechi za marudiano 5-6 na 12-13 Machi, 2019.

Comments are closed.