The House of Favourite Newspapers

Changudoa si kwa wanawake tu hata wanaume, sijui tuwaiteje?

0

Couple Relaxing In Bed Wearing PajamasAsalam alaikum wapenzi wasomaji wangu, wiki hii ndiyo ya kutekeleza lile agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Bila shaka wote tutafanya hivyo kuanzia vyumbani kwetu mpaka huko nje, kwani najua wazi kuwa mheshimiwa hawezi kukagua vyumba vyetu, basi mjihimu sasa na ule ukoko ulioko jikoni kwenye kuta zetu muutoe maana ni aibu kufanya usafi nje wakati ndani kuna tatizo.

Baada ya kuwaeleza hayo niingie moja kwa moja kwenye mada husika ambayo imebeba kichwa cha habari wanawake wengi wanaojiuza wanaitwa machangudoa lakini pia kuna wanaume wengine ambao tabia zao ni zilezile kama za machangudoa moja kwa moja nao ni machangudoa kama tu hawataachana na tabia hizi.

Mfano utakuta mwanaume anaamua kutembea na kila mwanamke pasipo kuangalia mwanamke anayetoka naye hii ni mbaya kiukweli, utakuta mwanaume anatembea na housigeli wake jikoni au bosi anatembea na mfanyakazi wake ofisini tena juu ya meza au kwenye uchochoro anambana baamedi bila kuangalia hadhi yake, huyu ataitwaje jamani?

Wanaume wengine hupenda kwenda ngomani kwa ajili tu ya kusaka wanawake ambao anajua atawavutia kwenye mgomba au mbuyu kisha atamaliza haja zake, sasa kwa hali ilivyo mbaya bila shaka kwa hili si sahihi na wanaume wote wenye tabia hii wanatakiwa kupewa majina.

Mada hii imekuja baada ya msomaji mmoja kuniandikia kuwa  anataka kuachana na mume wake kwani ameshindwa kabisa na tabia zake za kutembea na kila mwanamke bila kujua yeye ni mume wa mtu, hebu msikie mama huyu:

“Mimi ni mama mwenye watoto wawili na mume wangu wa ndoa tena ndoa yangu ni ya kanisani hivi ninavyokutumia ujumbe huu naona ndoa yangu imenishinda kiukweli kwani kila nikijaribu kumvumilia mume wangu  nashindwa, amekuwa ni wa kunibadilishia wanawake kama nguo, nikisafiri kidogo anaamua kuleta wanawake nyumbani kwangu bila hata haya na kulala nao hivyo nimeamua kuachana na maisha ya ndoa. Naomba ushauri wako.

Nilimpa ushauri mzuri mama R ambao kama ataufuata utamsaidia na ndoa yake haitavunjika, lakini niwape ushauri wanaume wenye tamaa hasa walio kwenye ndoa kuwa na staha. Kumbukeni mnapofanya mambo yasiyofaa vichochoroni, ofisini na maeneo mengine yasiyo rasmi mnawaaibisha wake zenu ambapo watu watawadharau kwa sababu mnashindwa kujiheshimu.

Kwa leo naishia hapa tuonane wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri.

Leave A Reply