Cheka, Alkasasu Kupasuana Usiku wa Mishindo

Bondia Cosmas Cheka akimtambia mpinzani wake mbele ya waandishi wa habari  hawapo pichani katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Atriums, Sinza, Dar.

MABONDIA wa ngumi za kulipwa nchini,  Muksini Swalehe ‘Alkasusu’ na Cosmas Cheka wanatarajia kupanda ulingoni  Desemba 3, mwaka huu katika pambano la usiku wa mishindo ambalo limepangwa kupigwa kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar.

 

Pambano hilo limetambulishwa leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika  kwenye Hoteli ya Atriums ambalo litashirikisha mabondia wengi, limeandaliwa na Kampuni ya Grobox Sports Promotion nchini ya  Siaha Mosha.

Promota wa pambano la Usiku wa Mishindo kutoka Grobox Sports Promotion, Siaha Mosha akizungumza mbele ya waandishi wakati akitambulisha pambano leo kwenye Hoteli ya Atriums, Sinza, Dar.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Promota wa pambano hilo,  Siaha  Mosha alisema kuwa wamezindua kampuni yao ambayo itakuwa inajihusisha na mambo ya burudani lakini kwa sasa wameanza na mchezo wa ngumi za kulipwa kwa kuwapiganisha Alkasusu na  Cheka katika pambano la Desemba 3, mwaka huu.

 

“Kitu cha kwanza ni kwamba tumezindua na kuitangaza kampuni  yetu ya Grobox Sports Promotion ambayo itakuwa ikihusisha na masuala ya burudani lakini kwa sasa tumeanza na mchezo wa ngumi ambao umekuwa mkubwa, tumeandaa pambano ambalo litawakutanisha Alkasusu na Cosmas Cheka kama pambano kuu.

“Pambano  linatarajia kufanyika Desemba 3, mwaka huu  na litajulikana kama usiku wa mishindo kwa sababu kila bondia anakishondo chake na kila mtu anataka kuacha historia, litakuwa ni pambano zuri na kubwa   na litafanyika kwenye Uwanja Kinesi, Dar,” alisema Mosha.

STORI NA IBRAHIM MUSSA | GPL

RAIS SAMIA AWAKA, MGAO WA MAJI DAR, ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA MIKOA – “MSITULAUMU”3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment