CHEKA TU: LEONBET EDITION yasimamisha jiji kwa burudani ya kibabe
Mashabiki wakubashiri wa kampuni inayotamba ya LEONBET Tanzania walipata burudani ya kisasa ya kuvunja mbavu na wachekeshaji maarufu nchini kwenye uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo uliopewa jina la CHEKA TU: LEONBET EDITION.
Burudani hiyo ya kisasa ilifanyika Novemba 8, 2024 kwenye ukumbi wa Warehouse Masaki.
Mashabiki wa vichekesho nchini walipata burudani kutoka kwa wakali wa Cheka Tu, akiwemo Coy Mzungu, Ndaro, Asma, Mtumishi Obama, na Chard Talent, ambao walihakikisha kuwa kila aliyehudhuria anatabasamu na kufurahia uzinduzi huo.
Burudani zaidi zilifuatia kwa muziki wa moja kwa moja kutoka kwa wasanii wakubwa wa Tanzania, akiwemo Maua Sama na Jaivah, ambao walifanya tamasha kuwa la kukumbukwa kwa mashabiki wote.
Katika tukio hilo, Meneja Mkuu wa LEONBET Tumaini Maligana pamoja Mkurugenzi wa Operesheni wa Kanda ya Afrika kwa LEONBET, Jérôme J. Dufourg katika burudani hiyo.
Viongozi hao wakuu wa LEONBET Tanzania waliwashukuru mashabiki wote waliofika katika uzinduzi huo na kuwapa sapoti kubwa.
Maligana, alitoa shukrani za dhati kwa wote waliojitokeza na kwa kuunga mkono uzinduzi wa brand yao.
“Ningependa kuchukua muda mfupi tu kuitambulisha brand yetu ya LEONBET – Simba La Mikeka. LEONBET ni kampuni ya michezo ya ubashiri iliyoingia rasmi Tanzania ili kuambatanisha burudani ya kubashiri kwenye michezo na slots na kutoa fursa ya kutengeneza pesa,” alisema,
Kwa upande wake, Dufourg, akiwakilisha mtazamo wa kimataifa wa LEONBET, alisisitiza dhamira ya kampuni hiyo ya kuleta uzoefu bora wa michezo ya kubashiri kwa Tanzania.