The House of Favourite Newspapers

Cheki Jumba La Kifahari La Staa Wa Movie Lilivyonusurika Kuteketea – Video

0

Nyumba ya kifahari ya dola milioni 26 sa na sawa na shilingi bilioni 65 za Kitanzania inayomilikiwa na muigizaji maarufu wa Hollywood, Tom Hanks, imeepuka kwa tundu la sindano moto mkubwa unaoteketeza maeneo ya Pacific Palisades.

Moto huu ambao umekuwa mwiba wa Los Angeles kwa siku kadhaa sasa umechoma zaidi ya ekari 17,000 za ardhi, kuharibu majengo zaidi ya 2,000, na kusababisha wakazi karibu 40,000 wa maeneo ya Malibu, Santa Monica, na Pacific Palisades kuhamishwa kwa dharura.


Katika picha za hivi karibuni zilizopatikana na vyombo vya habari, jumba la kifahari la Hanks limeonekana likiwa salama kabisa, lakini likiwa limezungukwa na nyumba kadhaa zilizotekeketea kwa moto huo.

Miongoni mwa nyota wengine waliokumbwa na janga hili ni pamoja na Paris Hilton, Anthony Hopkins, Tina Knowles, John Goodman, Candy Spelling, na Miles Teller, ambao nyumba zao zimeharibika kabisa. Moto huu wa kihistoria, uliobatizwa jina la Palisades Fire, sasa umeorodheshwa kuwa moja ya moto mbaya zaidi katika historia ya Los Angeles, ukiharibu zaidi ya ekari 34,000 za ardhi na kuvuruga maisha ya maelfu ya wakazi na watu mashuhuri.

Leave A Reply