Cheki Raisi Magufuli Alivyocheza Laivu Baada ya Kuzindua Kampeni

Katika kuonesha furaha na kuitumikia vizuri nchi yake na kufikia maendeleo ambayo wengi hawakuyatarajia Raisi Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuzindua kampeni za uchaguzi mkuu ambapo anawania kwa awamu ya pili alionekana kucheza laivu huku akiwa amejaa furaha na matumaini baada kuuona umati uliofurika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kumshangilia kwa shangwe kila alipowakumbusha aliyoyafanya.

Baadhi ya aliyowakumbusha ni pamoja na kuleta nidhamu kwenye ofisi za serikali, kuongeza idadi ya shule, hospitali na huduma nyingine.

Mengine ni kuzuia hutoroshwaji wa maliasili za taifa letu, ujenzi wa barabara za kisasa, madaraja pamoja na madaraja ya juu fly over, elimu bure na mengineyo.

Hayo ni baadhi ya mambo yaliyoshangiliwa sana wakati akiwakumbusha wananchi.

Ilikuwa ni furaha tupu.

Umati uliofurika ukishuhudia laivu.

Furaha ikiendelea.                                                                                                                                                            HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS GPL, Dodoma.

Toa comment