The House of Favourite Newspapers

Chelsea Bingwa FA, Yawachapa Manchester United bao 1-0

CHE LSEA jana ilitwaa ubingwa wa Kombe la FA, baada ya kuwachapa Manchester United bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Dimba la Wembley jijini London.

 

Huu ulikuwa mchezo wa mwisho kwa timu za Ligi Kuu England msimu huu na ubingwa huu unaweza kumfanya kocha Antonio Conte aongezewe mkataba mwingine kwenye timu hiyo na kupunguza presha ya kutimuliwa.

 

Staa wa Chelsea, Eden Hazard ndiye alikuwa shujaa kwenye mchezo huo baada ya kuifungia timu yake bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 22 ya mchezo huo, baada ya kuchezewa madhambi na beki Phil Jones.

Hata hivyo, baada ya bao hilo Manchester United walicharuka, lakini mashambulizi yao

mengi yalishindwa kuwapa bao na kujikuta wakimaliza mchezo huo bila bao.

 

Hata hivyo, dakika kumi za kipindi cha kwanza Chelsea walionekana kuwa bora sana huku wakikosa nafasi kadhaa za wazi.

 

Safu ya ushambuliaji ya Manchester United haikuwa na makali yaliyozoeleka baada ya kumkosa mshambuliaji wake, Romelu Lukaku ambaye alianzia kwenye benchi.

 

Kipindi cha pili, United ndiyo walionekana kukitawala huku wakipeleka mashambulizi ya nguvu langoni mwa Chelsea lakini hayakuzaa matunda.

Dakika ya 63, Alexis Sanchez aliifungia timu yake ya United bao lakini mwamuzi Mike Olvier akasema mfungaji ameotea baada ya kupata msaada wa kompyuta (VAR).

 

Hii ina maana kuwa Chelsea itacheza na Manchester City kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mwanzoni mwa mwezi Agosti ikiwa ni mchezo wa ufunguzi wa msimu wa ligi.

Hili ni taji la kwanza la Conte msimu huu na la pili tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo ya London mwanzoni mwa msimu uliopita, ambapo aliiongoza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.

 

Hata hivyo, ni kombe la nane la Chelsea la FA hali inayoendelea kuwaweka kwenye rekodi ya kati ya timu zilizotwaa ubingwa huo mara nyingi.

Comments are closed.