The House of Favourite Newspapers

Chelsea kama wanataka Ubingwa waachane na Goli Kipa wao

Nahodha wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher, amewaambia Chelsea kuwa kama wanataka kushinda ubingwa basi waachane na golikipa wake Roberto Sanchez, ikiwa ni baada ya wababe hao wa London kupoteza 2-1 dhidi ya Liverpool pale anfield hapo Jana.

Ilikuwa ni siku ngumu kwa Sanchez, ambaye alionekana kutokuwa na raha na mpira baada ya kufanya makosa yaliyopelekea kufungwa goli la pili na kwa maoni ya Carragher, alipaswa kufanya vyema zaidi kwa goli la ushindi la Jones.

“Kinachonikasirisha ni kwamba anapokwenda, anageuza uso wake ni kama anaogopa kugongwa na mpira, Rudi kwa Peter Schmeichel, na alipotoka, alifanya makubwa kubwa iwezekanavyo. Alisema Carragher

Na kuongeza kuwa “Yeye [Sanchez] anatokea kwa Curtis Jones ni Curtis Jones anapaswa kuwa na hofu kubwa kwamba mlinda lango anakuja kwake, yuko futi 6 na inchi 4, anakuja juu yake. Lakini yeye anaogopa mpira, Lazima ufike huko na matumaini mpira ugonge uso wako ili kuuzuia”.

Katika suala la kudhibiti mchezo, Chelsea walikuwa bora, lakini kilichowashinda ni mlinda lango,’ aliiambia Sky Sports

Sanchez licha kuonyesha uwezo mzuri katika baadhi ya michezo ikiwemo kuokoa penati dhidi ya Bournemouth, tayari amesharuhusu mabao 10 katika ligi kuu, huku timu yake ikishika nafasi ya 6 ikipoteza michezo miwili, kutoka sare michezo miwili na kushinda minne ikiwa na alama 14 mpaka sasa.