The House of Favourite Newspapers

Chelsea Kubadili Msimamo Wao na Kumvuta Ronaldo Darajani

0
 Nyota wa Manchester United Cristiano Ronaldo yupo a Timu ya Taifa ya Ureno katika mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar

KLABU ya Chelsea inaripotiwa huenda ikabadili msimamo wake na kufanya usajili wa nyota wa Manchester United na moja yaw achezaji bora wa muda wote wa mpira wa miguu duniani, Cristiano Ronaldo endapo tu Manchester United itamvunjia mkataba mchezaji huyo.

 

Kwa mujibu wa Gazeti la Daily Mirror, limeripoti kuwa Manchester United wapo katika hatrua za awali za kuvunja mklataba wa nyota huyo na kuwafanya Chelsea kufikiria uwezekano wa kumchukua nyota huyo katika kipindi cha dirisha dogo la mwezi Januari.

 

Klabu ya Manchester United inafikiria kuvunja mkataba wa Cristiano Ronaldo mapema kabla ya dirisha dogo la usajili mwezi Januari 2023

Ronaldo amepitia kipindi kigumu ndani ya kikosi hicho cha Manchester United chini ya kocha mpya Erik Ten Haag hali iliyosababisha kuikosoa vikali klabu hiyo kwenye mahojiano maalum aliyofanya na mwandishi wa Habari Piers Morgan.

Mmiliki mwenza wa klabu ya Chelsea Todd Boehly

Kwa sasa nyota huyo yupo na kikosi cha Ureno kinachoshiriki Mashindano ya Fainali za Kombe la Dunia nchini Qatar, na kwa mujibu wa ripoti kutoka vyanzo mbalimbali vya Habari za michezo barani Ulaya ni kuwa mpango wa Manchester United ni kutomruhusu Ronaldo kurudi katika viunga vya Carringthon mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Dunia.

Leave A Reply