Chelsea Kumtumia Werner Kama Chambo Kuinasa Saini ya Neymar, PSG Yataka Dau Nono

Neymar anaweza kuondoka kwenye kikosi cha PSG msimu huu

KLABU ya Chelsea ipo katika hatua nzuri ya kukamilisha dili la kuinasa saini ya Winga wa Paris Saint German Neymar Da Silva Junior kwa kitita cha Euro milioni 113 pamoja na Timo Werner kama sehemu ya dili hilo.

 

Kwa mujibu wa gazeti la habari za michezo la Italia Carciomercato limeripoti kuwa Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi amebariki dili hilo liendelee ingawa amesisitiza kuwa kiasi cha pesa lazima kiongezwe kutoka Euro Milioni 113 hadi 150 pamoja na Timo Werner ili kumruhusu Neymar kuondoka katika viunga vya Parc De Princes.

Luis Campos anadhamiria kumuondoa Neymar katika mipango ya klabu hiyo kwa msimu ujao

Habari za Neymar kutakiwa kuondoka ndani ya Klabu hiyo ya PSG zimepamba moto kwenye vichwa vingi vya magazeti na vyombo mbalimbali vya habari barani Ulaya huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni mipango ya Mshauri Mpya wa benchi la ufundi Luis Campos kuto ona umuhimu wa nyota huyo ndani ya kikosi hicho kwani anaamini hajitumi kuisaidia klabu hiyo.

Timo Werner mshambuliaji wa Chelsea anahusishwa kujiunga na PSG kwenye dili la kumpeleka Neymar Darajani

Campos aliyechukua mikoba ya Mbrazil Leonardo ni raia wa Ureno amabye amekuwa kwenye tasnia ya mpira wa miguu kwa miaka mingi huku akijikita Zaidi katika nafasi ya Ukurugenzi na ushauri wa masuala ya michezo kabla ya kujiunga na PSG alifanya kazi pia na klabu ya AS Monaco nayo ya nchini Ufaransa.

 

Kwa sasa inasubiriwa kuona kama Chelsea watakubali kutoa kiasi hicho cha pesa ili kukamilisha dili hilo la kumnasa Neymar ambaye ni moja ya nyota wenye majina makubwa katika soka Duniani.3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment