The House of Favourite Newspapers

Chelsea Mbioni Kumtangaza Vivell Kama Mkurugenzi Mpya wa Benchi la Ufundi

0
Christopher Vivell anatarajiwa kutangazwa kuwa Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi wa Klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza

KLABU ya Chelsea ya nchini Uingereza ipo mbioni kumtangaza Christopher Vivell kama Mkurugenzi mpya wa Benchi la Ufundi akitokea klabu ya RB Leipzig ya nchini Ujerumani.

 

Moja ya majukumu mama ya Vivell ndani ya klabu hiyo itakuwa ni kuhusika na sajili zote za timu kubwa pamoja na timu za vijana, kusimamia maendeleo ya soka kwa ngazi zote za klabu ikiwemo timu ya wanawake ya klabu hiyo pamoja na kusimamia mfumo mzima wa kusaka vipaji duniani.

 

Kwa mujibu wa mwandishi bora wa Habari za michezo duniani Fabrizio Romano, amebainisha kuwa suala la Vivell kutangazwa kuwa Mkurugenzi mpya wa Benchi la Ufundi Stamford Bridge ni suala la muda tu kwani taratibu zote zimeshakamilika.

 

“Ni Suala la muda tu.” alisema Fabrizio Romano kwa ufupi zaidi.

Vivell amepata umaarufu kutokana na kazi yake aliyoifanya ndani ya klabu ya RB Leipzig

Usajili wa Vivell ni moja kati ya sajili bora sana ndani ya klabu hiyo ambayo inafanya mabadiliko baada ya kuondoka kwa utawala wa aliyekuwa mmiliki wa zamani Roman Abramovich.

 

Todd Boehly mmiliki mwenza wa klabu ya Chelsea alipanga kumchukua Vivell kwa muda mrefu ambaye sasa anaingia kuungana na Joe Shields, Laurence Stewart pamoja na Paul Winstanley na wengine wengi ambao wanatakiwa kuajiriwa hivi karibuni.

Leave A Reply