The House of Favourite Newspapers

Chelsea Yahamishia Rada Zake kwa Winga Kinda wa Athletic Bilbao

0
Mshambuliaji kinda wa Athletic Bilbao, Nico Williams

HABARI kutoka katika viunga vya Stamford Bridge zinadai kuwa uongozi wa klabu hiyo umehamishia jitihada zake katika kuhakikisha wanainasa Saini ya winga kinda wa klabu ya Athletic Bilbao ya nchini Hispania, Nico Williams.

 

Nico Williams (20) anatajwa kuwa moja kati ya vijana wenye vipaji vya hali ya juu na ambaye anatarajiwa kfanya mambo makubwa katika soka kwa miaka ya hivi karibuni.

 

Usajili wa Nico Williams ambaye ni mdogo wa Inaki Williams unatarajiwa kugharimu kiasi cha Euro Milioni 50 na anatajwa kuingia majira ya dirisha dogo la usajili la mwezi Januari kuchukua nafasi ya Hakim Ziyech ambaye anatajwa kutimkia klabu ya AC Milan ya nchini Italia.

Leandro Trossard, nyota wa klabu ya Brighton na Timu ya Taifa ya Ubelgiji

Katika hatua nyingine klabu hiyo pia imepanga kukamilisha uhamisho wa nyota wa Brighton and Hove Albion Leandro Trossard ambaye pia anahusishwa na vilabu vya Manchester United pamoja na Liverpool.

 

Trossard anapewa chapuo kubwa la kutua Darajani kutokana na kuwa na uhusiano mzuri na aliyekuwa kocha wake ambaye kwa sasa ni Kocha wa Klabu ya Chelsea, Muingereza Graham Potter.

Leave A Reply