Chelsea Yaichapa Tottenham na Kutinga Fainali ya Carabao

Timu ya Chelsea imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la Carabao baada ya kuichapa Tottenham Hotspur bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya michuano hiyo, bao ambalo lilifungwa na Antonio Ruediger dakika ya 18 kwa assist ya Mason Mount

 

Mchezo wa kwanza uliopigwa darajani Stamford, Chelsea walishinda 2-0 na ushindi wa leo ugenini umewafanya kutinga fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla wa 3-0.

 

Chelsea sasa anamsubiri mshindi kati ya Liverpool na Arsenal watakaonza kumenyana katika nusu fainali ya kwanza Januari 13 katika dimba la Anfield kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa London juma moja lijalo.701
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment