testiingg
The House of Favourite Newspapers

Chelsea Yamfungia Kazi Winga wa Zamani wa Manchester United, Kutengeneza Pacha na Sterling

0
Wilfred Zaha akiwa na Crystal Palace

BAADA ya kukamilisha usajili wa winga wa Uingereza kutoka katika klabu ya Manchester City, Raheem Sterling klabu ya Chelsea imehamishia nguvu zake katika kutaka kuinyaka saini ya Winga wa Crystal Palace na Timu ya Taifa ya Ivory Coast Wilfred Zaha.

 

Habari zinadai kuwa Kocha wa Chelsea Thomas Tuchel ameliweka jina la Zaha kama kipaumbele kuelekea mwisho wa usajili na muda wowote ofay a kumnasa winga huyo mwenye kipaji cha hali ya juu inaweza kutumwa muda wowote.

Wesley Fofana, mlinzi wa kati wa klabu ya Leicester City

Tayari kumekuwa na mazungumzo ya kuwauza baadhi ya nyota wa klabu hiyo akiwemo Hakim Ziyech anayehitajika na klabu ya AC Milan, Timo Werner anayehitajika na Juventus pamoja na Christian Pulisic ambaye ameonesha nia ya kuondoka katika viunga vya Stamford Bridge.

 

Aidha klabu ya Chelsea inahusishwa na mpango wa kumnasa beki wa kati wa klabu ya Leicester City Wesley Fofana hiyo ikiwa ni baada ya kushindwa katika dili la kumsaini mlinzi wa kati wa Sevilla raia wa Ufaransa Jules Kounde ambaye anajiandaa kutimkia katika klabu ya Barcelona ya nchini Hispania.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Leave A Reply