Chelsea Yatangaza Kuachana na Mshauri wa Benchi la Ufundi Petr Cech

Mshauri wa zamani wa Benchi la Ufundi la Klabu ya Chelsea Petr Cech

KLABU ya Chelsea kupitia tovuti yake imetangaza kuwa mshauri wa benchi la ufundi Petr Cech ataondoka klabuni hapo mnamo Juni 30.

 

Tangu kuteuliwa kwake miaka mitatu iliyopita Cech amefanya kazi nzuri ya ushauri kwenye benchi la ufunsi ikiwa ni pamoja na kuongoza vyema masuala yote ya kimichezo huku akifanya kazi kubwa ya kuunganisha timu kubwa na ile ya vijana.

 

Cech amenukuliwa akisema:

Cech amewahi kuichezea Chelsea huku akipata mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya UEFA

“Imekuwa heshima kwangu mimi kufanya kazi katika nafasi hii na kwenye klabu kama hii ya Chelsea ukizingatia kuwa kuna uongozi mpya umeingia madarakani nadhani sasa ni waati sahihi kwangu mimi kuachia ngazi. Nimejisikia faraja kwamba klabu kwa sasa ipo katika mikono salama ya wamiliki wapya nan a uhakika itapata mafanikio makubwa ndani nan je ya uwanja.”

 

Mwenyekiti Mpya na Mmiliki mwenza wa klabu ya Chelsea Todd Boehly amesema:

 

“Petr ni mwanachama muhimu katika familia ya Chelsea. Tunaelewa uamuzi wake wa kuachia ngazi na tunamshukuru kwa mchango wake kama mshauri kwa maendeleo ya klabu na jamii yetu. Tunamtakia kila lakheri.”

 

 3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment