Chelsea Yazigomea Barca na Atletico

CHELSEA inadaiwa imezigomea Barcelona na Atletico Madrid zinazomgombea winga wake, Willian. Klabu hiyo inaaminika kuwa imekataa kumwachia winga huyo baada ya kumpoteza Eden Hazard, ambaye alijiunga na Real Madrid hivi karibuni.

 

Barcelona na Atletico Madrid inasemekana zilijitosa majuzi kwa Chelsea kwa ajili ya kumpata Willian. Klabu hizo inasemekana zilikuwa zimetoa ofa ya pauni milioni 35 (Sh. bilioni 101) ili kumpata winga huyo wa kibrazili.

 

Willian mwenye umri wa miaka 30 anatazamiwa kumaliza mkataba wa kuchezea timu hiyo baada ya kumalizika msimu wa 2019/20.

 

Chelsea imeweka ngumu kumuuza Willian kutokana na ukweli kuwa wamempoteza Hazard na pia wamefungiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Barcelona ndio timu ambayo kwa muda mrefu zaidi imekuwa inamwania Willian.

Loading...

Toa comment