The House of Favourite Newspapers

Chemical atambulisha Kagoma kwa mauno, amtaja Godzilla

MWANADADA anayetikisa katika Muziki wa Hip Hop Bongo, Claudia Lubao ‘Chemical’ ametambulisha ngoma yake mpya ya Kagoma huku akimwaga mauno kunogesha utambulisho huo.

 

Chemical aliyewahi kutamba na ngoma kibao kama Marry Marry na Asali akiwa na Beka Flavour alitambulisha ngoma hiyo ndani ya Bongo 255 kupitia +255 Global Radio inayoruka moja kwa moja kutokea mjengoni Global Group, Sinza Mori jijini Dar.

 

Mbali na kuitambulisha kwa mbwembwe ya kukata mauno,Chemical alisema video ya ngoma hiyo inayosubiriwa kwa hamuinatarajiwa kutoka Ijumaa hii ikiwa chini ya Dairekta Chriss.

“Kwanza nina mpango wa kuja na EP yangu (Extended Play au Albamu ya ngongeza) ambayo itakuwa na ngoma zangu kadhaa,” alisema Chemical.

 

Pia mkali huyo wa michano alizungumzia kuandika ngoma maalum kwa ajili ya marehemu Ngwair huku akisema kuwa aliyekuwa mkali mwingine marehemu Godzilla aliwahi kumsaidia sana katika muziki wake.

“Godzilla alikuwa kama kaka yangu, nilishaishi kwao nakumbuka nilikuwa nafanya mitihani ya chuo (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ‘UDSM’) kipindi hicho sina uhusiano mzuri na familia yangu kwa hiyo nilikuwa nikitokea kwa kina Godzilla naenda chuo kufanya mitihani yangu.

 

“Lakini pia nakumbuka nikiwa MJ Records (Kwa Master Jay) kwa mara ya kwanza nikiomba lebo kwa mara ya kwanza na nguo zangu za chuo alinisikiliza na kufanya naye ngoma. Nahisi ameondoka mapema wakati hata muziki bado haujamfanyia kitu,” alisema Chemical.

Imeandaliwa na Andrew Carlos/ GPL

Comments are closed.