The House of Favourite Newspapers

Chico Ampa Kiburi Nabi Yanga

0

KOCHA Mkuu wa Yanga, raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amesema kuwa ujio wa kiungo mshambuliaji,
Mkongomani, Chico Ushindi,
umeongeza ubora na ushindani wa namba katika kikosi chake.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Nabi alisema kuwa licha ya kuwepo hatihati ya kumtumia Fei Toto, lakini yupo Chico ambaye anamudu kucheza nafasi hiyo namba kumi.


Nabi alisema kuwa
anaamini uwezo mkubwa alionao Chico kutokana na kumfahamu baada ya kumfuatilia tangu akiwa klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.


Aliongeza kuwa Chico
ana uwezo wa kucheza nafasi zaidi ya moja namba 7, 10 na 11 hivyo uwepo wake katika timu, unampa nafasi kubwa ya kuwepo katika kikosi chake cha kwanza.


“Chico ana faida
kubwa katika timu, hiyo ni kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja katika timu, hivyo ninaamini atatoa mchango mkubwa katika timu.


“Hivyo ushindani
utaongezeka katika timu baada ya Chico kuja, hivi sasa kilichobakia kwake ni kuingia
katika mfumo
ambacho ni kitu kidogo, hilo ni jukumu langu ambalo nitalifanya,” alisema Nabi.

Leave A Reply