Chid Benz Aibukia kwa Diamond, Atoa Kauli Nzito Madawa ya Kulevya – Video
STAA wa Bongo Fleva ambaye amekuwa akihusishwa na matumizi ya madawa ya kulevya mara kwa mara hadi kukamatwa na polisi na kuwekwa ndani kisha kuachiwa, Chid Benz leo ameibuka katika sherehe za siku ya kuzaliwa ya msanii Diamond Platnumz na kuongea maneno ya magumu kuhusu dawa hizo baada ya kufanya shoo.
Sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Tandale zilihudhuria na watu mbali mbali wakiwemo viongozi wa serikali pia wadau mbali mbali wa sanaa ya muziki Tanzania. Chid benz alipata nafasi hiyo ya kuongea baada ya ku-perform wimbo wake ya “Dar es Salaam Stand Up” na kupokelewa kwa shangwe sana na wakazi wa Tandale waliohudhuria.
Chidi alimshukuru Diamond na wageni wote pamoja na mashabiki wake kisha akasema; “Madawa ya kulevya si mazuri lakini watu wanatumia na wanauza hii yote ni katika kutafuta hela, ila si kitu kizuri kama kinaweza kukusumbua ni vizuri kuachana nacho.
“Nashukuru kwa msaada wa Tale na Diamond kwangu, nashukuru sana kila kitu kiko sawa sasa cha msingi ni kufuatilia ili kupata maisha bora. Nashukuru kwa uongozi wa Wasafi kunipa nafasi, nafurahi kwa kila kitu kinachotokea hapa leo, kama wote tunakanyaga chini ya ardhi hakuna mtu anayeweza kupaa.” alisema Chid Benz.
Comments are closed.