Chid Benz, Q-Chilla Wakinukisha Tamasha la Wiki ya Usalama (VIDEO)

Q-Chila na Chid Benz wakikamua.

WAKONGWE kwenye game ya Bongo Fleva, Chid Benz na Q Chilla wamefanya makamuzi ya aina yake wakati wa Tamasha la Wiki ya Usalama Barabarani linalofanyika leo Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Shoo ikinoga.

Katika tamasha hilo lililoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi kitengo cha Usalama Barabarani likiwashirikisha wasanii mbalimbali wa muziki na filamu hapa nchini, lengo kubwa ni kutoa elimu juu ya usalama barabarani ili kupunguza ajali.

Chid Benz akipagawa.

Chila na Chid wamekiwasha huku wakishangiliwa maelfu ya mashabiki waliofurika kwenye Tamasha hilo.

Wanenguaji wakifanya yao.

Wakali hao wa tangu kitambo hicho, waliamsha hisia zaidi za mashabiki wao baada ya kugonga ngoma yao mpya ya Muda ambayo wameiachia hivi karibuni na kupokelewa vizuri sokoni.

Chid Benz na Chila wakisepa na kijiji.

Chila akikinukisha.

 

NA DENIS MTIMA | GPL

SHUHUDIA MAKAMUZI HAYO


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment