The House of Favourite Newspapers

Chikwende Aahidi Mabao Simba SC

0

PERFECT Chikwende, kiungo mshambuliaji wa Simba, amesema malengo yake ni kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye Kombe la FA na Ligi Kuu Bara, ambapo ameahidi kufunga mabao mengi kadiri anapopata nafasi.

 

Chikwende alikuwa katika kiwango bora katika mchezo wa Kombe la FA uliopigwa juzi Ijumaa dhidi ya African Lyon kwenye

Uwanja wa Mkapa, Dar ambapo alifunga bao moja dakika ya 62 akimalizia pasi ya Miraj Athumani katika ushindi wa mabao 3-0 walioupata Simba na kuisaidia timu yake kutinga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Akizungumza na Spoti Xtra, Chikwende amesema: “Kama mchezaji jukumu langu ni kuhakikisha napambana kuipa ushindi timu yangu, nimejipanga kufanya vizuri kwenye kila mchezo ambao nitapata nafasi, kama si kufunga basi nitengeneze nafasi kwa wenzangu, malengo yetu ni kutwaa ubingwa wa ligi pia Kombe la FA.

 

“Kikubwa mashabiki wetu wazidi kutupa sapoti kwenye kila mchezo na sisi tunawaahidi matokeo mazuri, sapoti yao ni muhimu sana kwetu.”

STORI: HUSSEIN MSOLEKA, Dar es Salaam

Leave A Reply