The House of Favourite Newspapers

Chikwende Anahitaji Muda Simba

0

KOCHA wa viungo wa Simba, Adel Zrane, amemkingia kifua kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mzimbabwe, Perfect Chikwende kwa kuweka wazi kuwa anaamini nyota huyo bado anahitaji muda zaidi ili kuzoea utamaduni wa Simba, ndipo afanye vizuri.

 

Chikwende alijiunga na Simba katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, mara baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo miwili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba.

 

Tangu atue Simba, Chikwende aliyekuwa akipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri, amekuwa akipata wakati mgumu kuingia kikosi cha kwanza, huku kukiwa na taarifa huenda akaachwa au kutolewa kwa mkopo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Zrane alisema: “Unajua namna ambavyo Chikwende alikuwa akicheza ndani ya FC Platinum ni tofauti kidogo na namna anavyocheza hapa Simba, kwa bahati mbaya hakuwa pamoja nasi katika maandalizi ya msimu, hivyo hata utimamu wake wa mwili haukuwa ule tulioutarajia.

 

“Wachezaji wote ndani ya kikosi cha Simba wana majukumu ya kushambulia, lakini pia wote lazima wasaidie kupunguza mashambulizi ya wapinzani kwa kukaba, lakini yeye akiwa Zimbabwe alikuwa mchezaji huru zaidi kwa kuwa hakuwa na majukumu ya kukaba, hivyo ni suala la kuzidi kumpa muda kukabiliana na hali hiyo.”

STORI:  JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave A Reply