The House of Favourite Newspapers

Chilala Ampoteza Zombi Ifakara

0
Bondia Saleh Mnamba akimchapa konde Yohana Aloyce katika pambano la raundi nne. Mnamba ameshinda kwa KO.

 

BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Charles Chilala wa Ifakara amefanikiwa kumkalisha vibaya kwa pointi mpinzani wake Innocent Kanuti ‘Inno Zombi’.

 

Promota Kepteni Seleman Semunyu akifanya mahojiano na mtangazaji wa Global Tv Online, Issa Liponda hapa kwenye Uwanja wa Taifa wa Ifakara.

Katika pambano hilo la raundi sita lililopigwa usiku wa kuamkia jana kwenye Uwanja wa Taifa wa Ifakara mjini hapa ambapo Chilala amecheza pambano kubwa akiwa bondia wa hapa Ifakara.

 

Chilala katika pambano hilo alicheza kwa kuonyesha umahiri mkubwa kuanzia katika raundi ya kwanza hali iliopelekea kushangiliwa muda wote na mashabiki waliokuwepo uwanjani hapo kushuhudia pambano hilo huku ikiwa ni mara yao kwanza kushuhudia pambano kubwa kwenye ulingo wa kisasa chini ya udhamini wa Global Tv Online, Smart Gin, Creative Bee na Peak Time Media.

 

Katika raundi ya nne ya pambano hilo, Chilala alifanikiwa kumpasua mdomo Zombi hali iliopelekea kutoka damu mdomoni kutokana na kumpiga mpinzani wake ngumi nyingi za usoni.

 

Hadi pambano hilo la raundi sita linaisha ambalo limehudhuriwa na bondia Selaman Kidunda, Mwanne Haji, Hassan Ndonga na Ismail Galiatano ambapo Chilala akatangazwa mshindi kwa ushindi wa majaji wote watatu.

 

Mara baada ya pambano hilo, Zombi alisema kuwa amepigwa kwa kuwa hakufanya maandalizi ya kucheza na Chilala lakini atakuwa tayari kuomba mechi ya marudiano ili kuweza kuonyesha ukubwa wake katika mchezo huo.

 

 

 

Kwa upande wa Chilala alisema ameshinda pambano hilo kwa kuwa alifanya maandalizi ya kutosha kwa lengo la kuwapa burudani wakazi wenzake wa Ifakara huku asisitiza wanatakiwa kupewa thamani inayostahili mjini hapo kwa kuaacha kuwakubeba mabondia wa kigeni badala yao.

 

Wengine walioshinda ni Haidari Mchanjo kwa TKO ya raundi ya tatu dhidi ya Festo Chiboni, Ayoub Mjeruman yeye amemtwanga kwa pointi Peter Ntinginya.

 

Washindi wengine ni Anuary Mlawa amemchapa Ibrahim Bakari, Saleh Mnamba akimtwanga Yohana Gerald na Fadhili Chamile akimpoteza Frank Likupellile.

Na Ibrahim Mussa, Ifakara

 

 

 

 

 

 

Bondia Frank Likupepulile akijaribu kumtwanga ngumi Fadhili Chamile. Chamile ameshinda pointi katika pambano la raundi nne.

 

 

Leave A Reply