China, Tanzania, Zambia Zakubaliana kuboresha reli ya TAZARA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping pamoja na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema leo Septemba 4, 2024 wameshuhudia uwekaji saini wa hati ya makubaliano ya kuboresha reli ya TAZARA katika ukumbi wa The Great Hall of the People jijini Beijing.