China Yagundua Kifaa Maalum cha Kutambua Wanaotazama Picha za Ngono

Kuangalia picha za utupu nchini China ni kosa kisheria

WATAFITI nchini China wamegundua kifaa maalum ambacho kitakuwa na uwezo wa kusoma akili, mawimbi ya ubongo au mvurugo wa kimihemko akilini wanaoupata watu hasa wanaume pindi wanapotazama picha (pilau) au videos (connections) za ngono (X).

 

Kwa mujibu wa mitandao mikubwa ya China, kifaa hicho kinavaliwa kichwani na kimeanza kuonesha matokeo mazuri baada ya wanafunzi wa kiume 15 wa chuo kufanyiwa utafiti wa kuvalishwa kifaa husika mbele ya kompyuta zinazoonesha picha za kikubwa.

Kifaa hicho kinaweza kubaini aliyeona na asiyeona picha za utupu

Taarifa hizo zinasema kuwa, kama mtu hajatazama picha za ngono matokeo ya kifaa hicho yatakuwa tofauti na yule ambaye ametoka kutazama, kwa hiyo kifaa husika kitasaidia kuwadaka wote wanaopenda kutazama videos za connections ili kukomesha wimbi kubwa la watazamaji wa videos hizo.

Kifaa hicho kinatumika kwa wanaume na wanawake pia

Nchini China kutazama connections za ngono ni kinyume na sheria hivyo mamlaka zimekuwa zikihaha kufanya juu chini kuondoa kabisa matumizi ya mapicha hayo machafu hasa kwa wanaume ambao tafiti zinaonesha ndio watazamaji wakubwa ingawa hata wanawake watadakwa na kifaa hicho ikiwa pia wametazama.

 

Cc; @sifaelpaul3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment