The House of Favourite Newspapers

China Yavunja Rekodi ya Kurusha Drone Nyingi Katika Onesho la City of Sky

0

Jioni ya Septemba 26, Shenzhen ilisherehekea onyesho la drones lililopewa jina la City of Sky, Maybe Shenzhen ambapo jumla ya drone ndogo 10,197 zilipaa angani kwa wakati mmoja.

Kitendo hicho kikaweka rekodi mbili za Guinness: “Idadi kubwa zaidi ya drones kurushwa kwa wakati mmoja na picha kubwa zaidi angani iliyoundwa na drones.

Katika rekodi hizo, China ilivunja rekodi yake ya awali, ya kurusha drone nyingi zaidi ambapo drone 8100 zilirushwa na kuweka rekodi ya Guiness.

Katika onesho hilo, kundi kubwa la drone lilitengeneza mandhari ya nyota angani, na kuwafanya watazamaji wahisi kama wanazunguka katika ulimwengu usio na mwisho.

Kilichowashangaza zaidi watazamaji jinsi drone hizo zilivyokuwa zinabadilika na kuonesha picha za mandhari tofautitofauti kila baada ya muda mfupi.

CHALAMILA AMUAMBIA RAIS SAMIA – ”DAR IPO SALAMA – HAKUNA JAMBO KUBWA LIMETOKEA LIMEATHIRI USALAMA”

Leave A Reply