The House of Favourite Newspapers

CHIPS HAZINA UKOKO

UNANISHA-NGAA wakati umes-hindwa kuyalinda maboga utaweza wapi matikiti! Haloooo eeeehhh wanakwambia kuvimba kwa mchele hakushtui mwiko shoga, upo nyonyo?

 

 Shoga kuna watu hawana tofauti na chafya, wakikutoka unashukuru unasema asante! Wengine wanajitia wapo juu juu kama nyama ya buchani wakati ni utumbo wa kibandani, heee heeiyaaa!

Leo nina udambwidambwi hadi natamani niwe juu juu kama feni ya panga boi, ukiniwasha tu nazunguka! Wareee reee! Hata niteme mate vipi koo linashindwa kunikauka shoga yangu nikipata meseji za hawa wanawake wenzangu ndiyo kabisaaa natamani dunia isimame nishuke miye!

 

Hivi kwa nini hamuishi visa! Mwanamke chapombe na baba naye chapombe mnategemea kuna maisha hapo? Mnategemea watoto watafuata tabia za nani hapo? Halafu bora sasa wangekuwa wanakunywa pombe kawaida, yaani wanakunywa wakiwa nyumbani wanashindwa hadi kuelewana kila mmoja na lugha yake! Aliyesema ukubwa wa kitambi hauvunji mguu na siyo kila mwenye mtoto ni mzazi wala hakukosea, mtu mzima na watoto juu lakini kutwa kuendekeza pombe tena wengine za kienyeji!

Jamani huu mwaka mpya na tunatakiwa kubadilika, hivi ukinywa kwa kiasi kuna tatizo? Utakuta mwanamke tena kapewa ofa tu basi kanywa kalewa kama siyo mke wa mtu au ana watoto wanaomtegemea, akirudi huko ndani ni kugombana mwanzo mwisho au watoto kuzoea hali ilivyo kisha wanahamishia tabia kwao!

 

Shoga naona koo linanikauka na mate sina, jamani chips hazina ukoko ndiyo maana huwezi kukuta zinageuzwa kiporo japo wanaofanya hivyo ndiyo hao ambao kunywa pombe kwao kupitiliza wameona dili hadi wanasahau kama wana familia. Mjumbe siku zote hauwawi, kwa leo niishie hapa shoga yangu, tukutane tena wiki ijayo kwa mada nyingine nzuri. Ni mimi Anti Naa Shangingi Mstaafu.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

 

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.