CHIRWA AJIUNGA AZAM FC – VIDEO

KLABU ya Azam imemtambulisha straika wake mpya, Obrey Chirwa kujiunga na klabu hiyo kwa kandarasi ya miaka miwili kufuati kuvunja mkataba wake na Nogotoom ya Misri ambayo alikimbilia baada ya kuondoka Yanga.

 

Azam FC walimalizana na straika huyo kwa ajili ya kuanza kuitumikia kwenye dirisha dogo ambalo litafunguliwa Novemba 15, mwaka huu.

Meneja wa Azam FC, Phillipo Alando amethibitisha na kusema: “Kuhusiana na jambo hilo na mambo mengine yote tutayazungumza kesho (leo) Alhamisi na watu watajua kutoka hapo. Tutaanika juu ya ligi pamoja na vitu vingine vinavyotuhusu, muhimu kufika katika mkutano huo wa waandishi” alisema Alando.

 

Chirwa amejiunga na Azam FC atakuwa amerudisha kombinesheni yake na mshambuliaji mwenzake, Donald Ngoma waliokuwa wote Yanga sambamba na kocha Hans van Pluijm.

CHIRWA Rasmi Azam Aungana na Ngoma Aikacha Yanga

Toa comment