The House of Favourite Newspapers

Chirwa amkimbiza straika Azam

Ujio wa Obrey Chirwa umesababi­sha Ditram Nchimbi aondolewe katika kikosi cha Azam.

Nchimbi alikuwa tegemeo kwenye kikosi cha Njombe Mji iliyoshuka daraja msimu uliiopita wa Ligi Kuu Bara kabla ya kusajiliwa na Azam, lakini ameshindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa akiwa Azam.

 

Kutua kwa Chirwa kumeongeza idadi ya washambuliaji kufikia sita, wengine wakiwa ni Donald Ngoma, Mbaraka Yusuph, Danny Lyanga, Yahya Zayd na Tafazwa Kutinyu, hiyo ni baa­da ya kuondolewa Nchimbi.

 

Meneja wa timu hiyo, Philipo Alando alisema kuwa wam­emtoa kwa mkopo Nchimbi kwenda ili akapate nafasi ya kucheza

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

Comments are closed.