The House of Favourite Newspapers

Chirwa Atua Dar Usiku

Obrey Chirwa.

MZAMBIA wa Yanga, Obrey Chirwa, amerejea nchini juzi Ijumaa usiku akitokea kwao, huku uongozi ukisisitiza kwamba kuna ishu wanaweka sawa kabla hajajiunga na wenzie Zanzibar.

 

Taarifa za awali zinasema kwamba mchezaji huyo alikuwa amesusa akitaka kumaliziwa chake alichokuwa akidai kwenye fungu la usajili, ingawa zipo taarifa pia kuwa alishindwa kurejea kwa wakati Dar es Salaam baada ya Yanga kushindwa kumtumia tiketi.

 

Mchezaji huyo alionekana kwenye picha tofauti akijihusisha na kilimo alipokuwa kwao huku wenzie wakiendelea kupiga mzigo. Katibu Mkuu ya Yanga, Charles Mkwasa, ameliambia Spoti Xtra kuwa; “Chirwa amerejea alipokuwa ameenda baada ya kupata matatizo ya kifamilia, kwa hiyo muda wowote atakapomalizana na uongozi atakwenda Zanzibar kujiunga na timu.”

 

 

“Kuna baadhi ya mambo yake yalikuwa hayajakaa sawa ambayo siwezi kuyasema lakini yakiisha kuwa sawa ataenda Zanzibar kuungana na wenzake,” alisema Mkwasa. Alipoulizwa kuhusiana na fedha za usajili ambazo Chirwa anaidai klabu hiyo Mkwasa alisema: “Suala hilo kwa sasa siwezi kulizungumzia ila ninachoweza kusema ni kwamba tunadaiwa na wachezaji wengi na taratibu za kuwalipa zinaendelea kufanyika.”

STORI NA SWEETBERT LUKONGE NA MARTHA MBOMA

Comments are closed.