The House of Favourite Newspapers

CHOCKY AFUNGA NDOA KIMYAKIMYA

Chocky na mkewe wa pili (kulia), Zai;  kushoto ni mkewe wa kwanza Addat Pinket.

MWANAMUZIKI, Ali Chocky,  ameoa mke wa pili aitwaye Zai Kingo na kufunga naye ndoa jijini Dar.

 

Akizungumza na Global Publishers, Chocky ambaye kwa sasa anafanya shughuli zake za muziki jijini Mwanza, alisema aliamua kufunga ndoa hiyo kimyakimya jana kwani ameona ni muda muafaka wa kuhalalisha ndoa.

 

“Si unajua tena utu uzima huu nikaona ni vyema nifanye kitu japo kuhalalisha tu, sikutaka iwe sherehe kubwa wala nini, kiasi tu cha mimi, mke wangu na watu wachache sana. Mke wangu huyu kabla ya kumuoa nilishakuwa naye kwa takriban miaka miwili hivi,” alisema Chocky.

 

Chocky alisema anamshukuru Mungu baada ya kuugua kwa muda mrefu, kwa sasa yupo fiti na anafanya makamuzi ndani ya Jiji la Mwanza,  hivyo mashabiki wake waendelee kumuunga mkono.

 

Stori: Erick Evarist

BONGO MUVI Waamua Kumfata MSUKUMA Bungeni “Kauli Imetuumiza”

Comments are closed.