The House of Favourite Newspapers

Choki Afungiwa Twanga Miezi Miwili

0

Issa Mnally na Richard Bukos |CHAMPIONI| GPL
BENDI ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ ya jijini Dar, imempiga stop mwanamuziki wake nyota Ally Choki asipande jukwaa la bendi hiyo kwa muda wa miezi miwili.
Akizungumza na Championi Jumatatu, mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo ambaye hakupenda kutajwa jina, alisema uongozi wa bendi hiyo ulio chini ya mwanamama Asha Baraka, umemsimamisha mwanamuziki huyo kwa muda wa miezi miwili.
“Nakuomba usinitaje lakini habari za uhakika nakupa Choki amesimamishwa kupanda jukwaa lolote lile wanalopiga Twanga kwa muda wa miezi miwili kwa maana hiyo ataonekana katika maonyesho yetu kuanzia mwezi wa saba,” alisema.
Mtoa habari huyo ametaja sababu ya kusimamishwa kwa Choki kuwa ni tabia yake ya kutohudhuria baadhi ya maonyesho ya bendi hiyo na kujihusisha sana na kazi zake za nje.
Alipotafutwa Choki, alithibitisha kusimamishwa kwake kwa muda wa miezi miwili. “Kweli nimesimamishwa, jamani si unajua mama (Asha Baraka) anapenda sana kusikiliza vitu vya uongo na kuvichukulia maamuzi ya jazba!” alisema Choki.
Meneja Mkuu wa bendi hiyo, Hassani Rehani alithibitisha: “Ndiyo tumemsimamisha kutokana na kukithiri kuomba ruhusa mara kwa mara za kufanya maonyesho yake binafsi, tumempa miezi miwili amalize kwanza hizo ‘ndondo’ zake.”

Leave A Reply