Chongolo Aanza Ziara Mkoani Manyara Kupokea na Kutatua Kero za Wananchi
SEKRETARIETI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo leo imeanza ziara mkoani Manyara ya kupokea na kutatua kero za wananchi.
Ziara hiyo pia inalenga kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Akiwa katika Wilaya Hanang Kijiji cha Hirbadaw kwenye mkutano wa shina namba 16 Chongolo amesema CCM imedhamiria kukatua kero zinazowakabili wananchi ili zisikwamishe wao kujiletea maendeleo.
Awali, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Sophia Mjema amehimiza viongozi wa mashina kuwa na mikutano ili kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Naye, Katibu wa NEC, Idara ya Organizesheni, Issa Gavu, amesema CCM ndio yenye uwezo wa kutatua matatizo ya wananchi kutokana na mipango na dhamira iliyonayo.