Chongolo Amwapisha Elias Mwandobo Kuwa Mkuu Mpya wa Wilaya ya Momba
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemwapisha Mkuu Mpya wa Wilaya ya Momba, Elias Mwandobo, uapisho uliofanyika Juni 14,2024 katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Nselewa, Mbozi mkoani Songwe.
Chongolo ametoa maagizo saba kwa Mwandobo kwenda kuyatekeleza ikiwemo kuhakikisha usalama unaimarishwa katika wilaya hiyo hasa katika mpaka wa Tunduma ili kuimarisha uchumi wa wilaya na mkoa pamoja na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ikiwemo migogoro ya wakulima na wafugaji.
Chongolo amesema hayo mara baada ya kumuapisha Mwandobo aliyeteuliwa Juni 11, 2024 akichukua nafasi ya kenani kihongosi aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Pamoja na hayo, Chongolo amemtaka Mwandobo kuhakikisha anaendeleza utekelezaji wa afua za lishe ili kupunguza udumavu hii ikiwa ni agenda ya mkoa kutokana na Mkoa wa Songwe kuwa miongoni mwa mikoa yenye kiwango kikubwa cha udumavu.