The House of Favourite Newspapers

Chongolo Awanyooshea Kidole Watendaji wa Serikali, Akemea Migororo ya Ardhi

0

 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amewanyooshea kidole watendaji wa serikali kwa kuwa na tamaa za kutaka mafanikio ya haraka badala ya kkujiusisha na shughuri za utafutaji maendeleo katika maeneo ya kazi waliyopangiwa

 

Akiongea na wakazi wa kata ya Dakawa Wilaya ya Morogoro katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho Cha CCM Chongolo amesema wilaya hiyo imekuwa ikipitia migogoro ya Ardhi kutokana na baadhi ya watendaji kuwa wafugaji

 

 

“Unakuta leo mtu anapewa kazi ya kuwa mtendaji wa Kata kesho unamkuta anamiliki ng’ombe ishirini, mshahara wake hata kwa mwaka hauwezi kumfanya kuwa na Ng’ombe wawili,” amesema na kuongeza Kusema Sasa “Niwatakemewataka watendaji wote wa serikali kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi yao.

 

Hata hivyo pamoja na kuwataka watendaji kuzingatia maadilina Miikao ya kazi zao, amewataka wafugaji kuacha kupeana mialiko katika maeneo wanayopangiwa na serikali kwa ajili malisho.

 


“Ukiona kuna mgogoro wa Mkulima na Mfugaji maana yake kuna mtu hapo katikati anategeneza tatizo hivyo basi Serikali imekuwa ikiweka utaratibu wa mpango bora wa matumizi ya ardhi kwa kutenga maeneo kwa ajili ya kilimo ,wafugaji,”

Nakuogeza Kusema” Lakini kumekuwa changamoto kwa wafugaji wanaalikana wengi baadae eneo linakuwa dogo wanaingia kwa mkulima migogoro inaanza huku mkulima ukimpa eneo lake atalima kama alivyohitaji,” amesema Chongolo.

Kutokana na hali hiyo Chongolo amemtaja Mkuu Wilaya ya Mvomelo Dkt, Judith Lundi kuhakikisha anapunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika Wilaya yake.

Awali Mbunge wa Jimbo hilo Jonas Vanzela ametoa malalamiko kuwa Wilaya hiyo imekuaa na migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na migogoro ya mipaka.

Leave A Reply