The House of Favourite Newspapers

CHOO CHA SHULE CHAPOROMOKA, MTOTO MMOJA AJERUHIWA – PICHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU TUKIO LA KUTITIA KWA CHOO KATIKA SHULE YA MSINGI SELIAN ARUMERU

Leo 26/10/2018 majira ya saa 3:00 asubuhi tumepata changamoto ya kutitia na kuanguka kwa jengo la choo cha Shule ya Msingi ya Seliani katika Kijiji cha Olevolosi, Kata ya Kimnyaki, Wilaya ya Arumeru ambapo katika tukio hilo tumemwokoa mwanafunzi mmoja wa kiume aliepata majeraha lakini bado tunaendelea na jitahada za kuondoa kifusi kilichochanganyikana na matofali ambacho kimezama katika shimo la choo hicho kilichokuwa na matundu 20.

 

 

Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro akiambatana na Katibu Tawala wa Mkoa na viongozi wa Halmashauri ya ARUSHA walifika eneo la tukio na kuanza jitihada za uokoaji wakishirkiana na Vikosi vya Uokoji na Zimamoto pamoja na mamia ya wananchi wa Kata ya kimnyaki.

Katika jitihada hizo, walifanikiwa kumuokoa mwananfunzi mmoja akiwa amejeruhiwa usoni na kukimbizwa katika Hospitali ya Seliani kwa matibabu zaidi ambapo mpaka sasa vikosi vya uokoaji vinaendelea na jitihada zaidi ambapo choo hicho ndicho kilikuwa choo pekee kilichokuwa kikitumiwa na zaidi ya wanafunzi 1,121 wa shule hiyo.

Katika eneo la tukio kwanza tulilazimika kurejesha hali ya amani na kutuliza taharuki za wananchi ambao baadhi wana watoto wanaosoma katika shule hiyo na kutoa nafasi kwa vikosi vya ukoaji kuendelea na zoezi la kutafuta wanafunzi wengine kutokana na kutokupatikana kwa Taarifa za awali zinazoonyesha idadi ya wanafunzi ambao huenda walikuwa kwenye choo hicho.

Kutokana na shule hiyo kuwa na choo kimoja, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru alilazimika kuchukua hatua za kuzungumza na Uongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Seliani na kuomba shule kutumia vyoo vya Kanisani ombi ambalo lilikubaliwa na Mkuu wa Jimbo la Arusha Magharibi, Mchungaji Philemon Joseph Mollel na kuondoa Mashaka ya kufungwa kwa shule.

Muro alizungumza na wananchi waliojitokeza ambapo katika na kuwataka wananchi hao kutulia na kutoa fursa ya kuendelea kwa zoezi la utoaji wa kifusi ili kujirisha na madhara zaidi ambayo huenda yametokea.

Awali, kwa upande wao baadhi ya wananchi waliungana na Mkuu wa Wilaya katika kuchanga fedha kwa ajili ya kuanza Mikakati ya Ujenzi wa choo kingine ili kutokwamisha masomo ya wanafunzi kazi ambayo ilifanywa na Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wa Kanisani na halmashauri na kuitikiwa kwa wingi na wananchi wailiotoa Fedha zao.

Muro alimtembelea mwanafunzi majeruhi ambae amelazwa katika hospitali ya seliani na kumjulia hali uku akiongozana na viongozi mbalimbali.

Imetolewa na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
26/10/2018

 

Comments are closed.