Chris Brown: msijisumbue, nakuja kufanya shoo
Mwanamuziki wa muziki wa RnB, Chris Brown.
New York, Marekani
MKALI wa muziki wenye mahadhi ya RnB, Chris Brown, ameibuka na kujibu zile taarifa zilizotoka kuwa kawekewa ngumu kwenda Australia kwa ajili ya kufanya shoo Desemba, mwaka huu kwa kusema: “Nakuja”.
Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwepo taarifa kwenye mitandao mbalimbali kuwa staa huyo wa Kibao cha Royal, amewekewa ngumu kwenda nchini humo kufanya shoo kwa madai ya kumdhalilisha aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna kwa kumpa kipigo, mwaka 2009.
Mitandao hiyo ‘ilimkoti’ Waziri wa Wanawake wa Australia, Michaelia Cash, akitaka kupeleka pendekezo kwa Waziri wa Uhamiaji wa nchi hiyo, Peter Dutton ili asimpe kibali Chris cha kutua nchini humo kutokana na kutomuheshimu mwanamke (Rihanna).
Kupitia mtandao wake wa Facebook ambao anatumia jina la Chris Brown wenye ‘like’ 39,88,648, msanii huyo alisema kuwa taarifa za kukataliwa kwake ni za uongo hivyo atatimba kama kawaida kwenye shoo hiyo na kuongeza kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikipotosha ishu hiyo, lakini baadaye akaifuta haraka ‘status’ hiyo.
Hata hivyo, Serikali ya Australia na ile ya New Zealand ambako Chris ana ‘tour’ aliyoipa jina la One Hell Of A Nite, ametakiwa kutoa maelezo kwa nini apewe kibali cha kuingia nchini humo ndani ya siku 28.