Mwanamke Mwingine Amemshitaki Chris Brown

MWANAMKE  mmoja anayetambulika kwa jina la Danielle Griffin amemshitaki Chris Brown baada ya kuteseka na maumivu ya macho kwa kipindi ch zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Kwenye maelezo yake, Danielle amedai kuwa alichukuliwa kama mtu wa kucheza muziki kwenye moja ya video za Breezy ambayo ilifanyika mwishoni mwa mwaka 2017 pande za Los Angeles, Marekani. Kwa mujibu wa tmz, ilitokea wakati mtaalam wa mapambo (Make-Up Artist) alipommiminia damu feki mrembo huyo ambaye baada ya muda alianza kusikia maumivu ambayo yamedumu kwa muda mrefu na kumsababishia matatizo ya kuona.

Mwanasheria wa mrembo huyo ameiambia tmz kuwa Danielle ametembelea hospitali tatu tofauti kwa ajili ya kutibu majeraha yake kwa miezi mitatu mfululizo, kitu ambacho kilimsbabishia aache masomo yake na kukosa nafasi nyingi za kazi.


Loading...

Toa comment