The House of Favourite Newspapers

Christian Eriksen Hafikirii Kuondoka Tottenham

Kiungo wa Tottenham Hotspur, Christian Eriksen.

KIUNGO wa Tottenham Hotspur, Christian Eriksen amesema hafikirii suala la kuondoka timu hiyo bali anawazia kushinda mataji.

 

Kiungo huyo mahiri amekuwa anafuatiliwa na vigogo vya soka barani Ulaya.

Barcelona imetajwa kama miongoni mwa klabu zinazotaka kumsajili nyota huyo.

 

“Kusema ukweli sifuatilii mambo ya timu zinazonihitaji lakini akili yangu zaidi ipo kuisaidia Tottenham kutwaa mataji,” alisema Eriksen, ambaye anategemea kuongezewa mkataba na Tottenham hivi karibuni.

Comments are closed.