Chuchu Ajifungua Kidume

 

Chuchu-Hans

Staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans.

STAA wa filamu Bongo, Chuchu Hans, hatimaye amejifungua mtoto wa kiume katika Hosptali ya Taifa ya Muhimbili,  akiwa mwanamke wa kwanza kumpatia muigizaji mkubwa kiume  Vincent Kigosi ‘Ray’, mtoto.

chuchu2.jpg

Chuchu Hans akiwa na mpenzi wake Vincent Kigosi ‘Ray’.

Akizungumza Mtanda huu ndugu wa karibu na mastaa hao alithibitisha kujifungua kwa Chuchu na kusema kuwa ujio wa mtoto huyo ambaye wamempa jina la kwanza la Vincent Junior, kuwa ameleta furaha kubwa kwa  Ray.

“Yaani Ray, alikuwa Zanzibar kwa ajili ya kungalia mpira lakini alipopata habari hiyo alionekana mwenye furaha sana huku baadhi ya mastaa wenzake wakimpongeza,” alisema ndugu  huyo.

(Na Imelda Mtema/GPL)


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment