The House of Favourite Newspapers

Chuchu aweweseka kuwa mbali na Ray

0

chuchuImelda Mtema

MAHABA popote! Msanii nyota wa sinema za Bongo, Chuchu Hans ametoa dukuduku lake la moyoni akisema kwamba, anamkumbuka sana mchumba wake ambaye pia ni msanii wa filamu, Vincet Kigosi ‘Ray’ ambapo kwa sasa wapo mbalimbali kutokana na misafara ya kampeni za siasa kuelekea uchaguzi mkuu, Oktoba 25, mwaka huu hivyo kumfanya aweweseke.

RAY (1)Akichezesha taya na Amani juzi, Chuchu alisema kwa kipindi chote cha kampeni ambacho Ray yuko na wasanii wenzake kwingine na yeye yupo sehemu nyingine, wanazunguka mikoani amekuwa akimkumbuka

sana mpenzi wake huyo lakini hana jinsi.

“Yaani kiukweli nimemkumbuka sana baby wangu, sema tu kila mtu anapiga kazi mwisho wa siku maisha yanakwenda sawa na tunashukuru karibu tunamaliza kampeni, hivyo tutakutana tena. Kweli nimeamini kupenda ni hatari,” alisema Chuchu.

Leave A Reply