The House of Favourite Newspapers

Chuchu Hans aanika siri ya kumkoleza Ray

0

RAY (1)NINA imani mu-wazima wa afya wasomaji wetu, kama kawa kwenye kolamu hii tumekuwa tukiwaleta mastaa tofautitofauti na kufunguka mambo mbalimbali yahusuyo maisha yao kwenye sanaa na nje ya fani.

Leo tunaye staa wa filamu Bongo, Chuchu Hans ambaye ni mwandani wa msanii mkongwe kwenye ulimwengu wa filamu Bongo, Vincent Kigosi `Ray’ aliyeweza kufunguka mambo mbalimbali kutokana na maswali aliyoulizwa na wasomaji wetu katika kolamu hii wiki iliyopita na kuyatolea ufafanuzi bila hiyana.

Msomaji: Unamzungumziaje Jackline Wolper kukuponda kisa kuhama Ukawa? 0758 476733.

Chuchu: Nimejisikia kawaida tu sababu Wolper hawezi kuingilia maamuzi yangu na huo ni msimamo wangu.

Msomaji: Ni aina gani ya gari unayoipenda mama Kigosi? 0657 689250.

Chuchu: Hahaaa siyo siri naipenda sana BMW  ndiyo inayoninyima usingizi.

Msomaji: Dada Chuchu nasikia unatokea Tanga mapenzi yanapozaliwa, japo mnasifika sana kwa ufundi watoto wa Kitanga lakini mambo ya ndumba nayo yanahusika kuwadatisha wapenzi wenu, vipi wewe hujafanya mambo ya kienyeji na dua kumteka Ray? 0684 899791.

Chuchu: Hakuna kitu kama hicho mapenzi yangu na Ray yanadumishwa na ukarimu wangu ninaomuonyesha, kwa kifupi ni jinsi tunavyoishi kutokana na usikivu na uelevu.

Msomaji: Bila kuficha wewe ni mzuri kuanzia sura mpaka kazi zako, lakini kwa nini umekuwa kwenye migogoro na Johari kwa sababu ya kumchukulia Ray.

0657 042001.

Chuchu: Mimi sina migogoro na mtu.

Msomaji: Naitwa Naima dada naishi Upanga kiukweli napenda sana kazi zako, mimi pia napenda sana kuigiza lakini sijui pa kuanzia nahitaji msaada wako.

0713 866015.

Chuchu: Watu wa aina hiyo mpo wengi, kwa sasa nipo bize kuna mambo nayaweka sawa, zikitokea nafasi nitatangaza.

Msomaji: Dada Chuchu napenda sana kazi zako, kwenye mahusiano ulishawahi kutendwa na ulichukua maamuzi gani? 0782249126.

Chuchu: Kutendwa kupo ni jambo la kawaida katika zama hizi tofauti na kipindi cha nyuma cha wazee wetu, nilikubali matokeo nikaamua kukaa chonjo.

Msomaji: Ninavyofahamu ulikuwa na mumeo wa ndoa mliachana au, kitendo cha kuwa na Ray huoni umemdhalilisha mumeo? 0715 066640.

Chuchu: Hayo ya kuwa na Ray ni maamuzi yangu binafsi, lakini mume tumeshaachana.

Msomaji: Napenda sana kazi zako wewe dada pia ni mrembo, hivi ni kweli ulifuata pesa Ukawa? 0676 373165.

Chuchu: Si kweli, Wolper alijisikia kuongea kufurahisha mdomo wake siwezi kumkataza, kuhama chama ni jambo la kawaida niliamua tu na sioni cha ajabu katika hilo mbona hata viongozi wanahama vyama.

Msomaji: Hongera kwa kazi zako napenda unavyoigiza, nakushauri umzalie mtoto Ray maana umri unaenda. 0754857575.

Chuchu: Hakuna shida, Mungu akipenda nitamzalia maana kila jambo linapangwa na yeye kwa wakati wake aliokusudia.

Msomaji: Dada nakukubali sana, vipi elimu yako? 0714 403227.

Chuchu: Niliishia kidato cha sita kisha nikasoma kozi mbalimbali ikiwemo Hotel Management, lakini

Leave A Reply