Chuchu Hans asema hajawahi kukerwa na mitandao

LICHA ya kuandamwa mara kwa mara na mitandao ya kijamii kwa skendo mbalimbali, mwanamama mwigizaji wa filamu za Kibongo, Chuchu Hans amesema hajawahi kukerwa na maneno mabaya yatolewayo na mashabiki kwenye mitandao.  Akistorisha na Shusha Pumzi mapema wiki hii alipokuwa akisheherekea siku yake ya kuzaliwa, Chuchu alisema watu wamekuwa wakimtolea kauli chafu na mbaya kwenye mitandao ya kijamii, lakini hajawahi kujali wala kukereka nayo.

“Watu wamekuwa na kawaida ya kuwasema vibaya wenzao bila kujali na kujua ni jinsi gani wanaumizwa na hayo maneno yao, lakini mimi sijali kwa sababu nimeshachagua kuwa maarufu kwa maana hiyo najua nitaongelewa tofauti na watu,” alisema Chuchu

STORI: AMMAR MASIMBA


Loading...

Toa comment