The House of Favourite Newspapers

Chuchu Hans: La kuolewa halipo akilini mwangu!

chuchu.jpgKAMA kawaida kwenye kolamu hii tunawaletea mastaa mbalimbali na kuwabananisha kwa maswali kumi. Leo tunaye staa wa filamu Bongo Chuchu Hans ambaye anabanwa na Mwandishi Wetu Mayasa Mariwata, ikawa hivi;

Ijumaa: Ningependa kujua ukiwa nyumbani na mpenzi wako unapenda kumpikia vyakula gani?

Chuchu: Napenda sana mapishi kuliko chochote, nikiwa nyumbani napendelea kupika wali wa nazi na samaki. Ni chakula kinachonivutia zaidi mimi na mwandani wangu.

Ijumaa: Wasanii wengi wanapenda kujichubua wakiamini wanaongeza urembo, wewe ni miongoni mwao?

Chuchu: Mimi na mkorogo ni vitu viwili tofauti, nauchukia! Hao wanaojichubua hawajiamini, siri kubwa ya urembo wangu ni kula kwa mpangilio na kupata muda mzuri wa kupumzika.

Ijumaa: Kutokana na muonekano wako, ni mavazi gani ambayo unaamini ukivaa yatakufanya uwe amazing?

Chuchu: Nguo yoyote ile ambayo nikivaa nihakikishe imenipendeza, ila navutiwa zaidi na nguo ndefu.

Ijumaa: Kumekuwa na maneno yasiyochuja kuwa wasanii wengi wanatumia dawa za Kichina kuongeza shepu, likoje hilo na wewe hujawahi kufikiria kitu hicho?

Chuchu: Ninachojua wengi wanavaa zile taiti za Kichina ambazo mtu anaonekana kajazia. Mimi wala sifikirii hayo, najikubali nilivyo.

Ijumaa: Tunajua uko na Ray, kuna madai huwa unachepuka, hilo likoje?

Chuchu: (Kicheko) hapana bwana, najiheshimu sana kuliko watu wanavyofikiria.

Ijumaa: Ni changamoto gani uliyowahi kukutana nayo ukajikuta unajuta kuwa staa?

Chuchu: Changamoto zipo nyingi, ila kubwa kuliko ni kukosa uhuru katika maisha maana kuna mambo unalazimika kufanya hata kama hayaendani na uwezo wako.

Ijumaa: Unapenda kuwa na watoto wangapi katika maisha yako?

Chuchu: Siwezi kukadiria idadi ya watoto kwa kuwa kila jambo anapanga Mungu.

Ijumaa: Endapo ukiolewa na Ray, utapenda mapumziko yenu ‘honeymoon’ yawe nchi gani?

Chuchu: Hilo la kuolewa haliko akilini mwangu kwa sasa.

Ijumaa: Ni maungo gani ya mwili wako ukiguswa unadata zaidi ukiwa kwenye dimbwi la mahaba?

Chuchu: Hayo ni mambo ya siri siwezi kuyaanika ila zipo hizo sehemu ‘amazing’ sana.

Ijumaa: Kuna kipindi nilisikia umekorofishana na Ray tatizo lilikuwa nini?

Chuchu: Yalikuwa maneno ya watu tu, mkipishana kidogo ooo wamekorofishana, hakukuwa na ishu kubwa.

Ijumaa: Unazungumziaje haya mabifu ya mastaa kisa kuibiana wanaume?

Chuchu: Ni mambo ya kijinga tu na wanaofanya hivyo ni malimbukeni wa maisha.

Comments are closed.