Chuchu Hans: Nitazaa na Wanaume Wangapi?
MWANAMAMA mrembo kunako gemu ya filamu nchini Chuchu Hans, amesema kuwa wanaume wengi huwa wanamfuata Dm katika ukurasa wake wa Instagram nakumuomba awazalie.
“Nitazaa na wanaume wangapi jamani? Mimi huwa nashangaa jinsi wanaume wengi wanavyonifuata na kuniomba nizae nao.
“Kuna wengine wamekuwa wakiniahidi kunipa fedha nikiwakubalia kufanya hivyo, mimi siwezi watoto nilio nao wanatosha na nampenda mpenzi wangu,” alisema Chuchu.
Mara kadhaa watu wamekuwa wakimtaja mwanadada huyu kuwa na damu ya kuzaa watoto wazuri pengine ndiyo sababu ya wazee wa fursa wanayotaka kuitumia kujipatia uzao kwa mwanamke huyo ambaye ni manzi wake na staa Ray Kigosi.
Stori: Memorise Richard


